Top Songs By Ambwene Mwasongwe
Similar Songs
Credits
AUSFÜHRENDE KÜNSTLER:INNEN
Ambwene Mwasongwe
Künstler:in
KOMPOSITION UND LIEDTEXT
Ambwene Mwasongwe
Songwriter:in
PRODUKTION UND TECHNIK
Thimos Chelula
Produzent:in
Lyrics
[Verse 1]
Mlilelewa na wazazi sasa mmekua
Ndio maana mmeamua kuanza maisha yenu
Mmeacha baba na mama kuwa mwili mmoja
Ndoa yenu ni takatifu mtu asiwatenge
Bila shaka mmejifunza mambo mbalimbali
Japokuwa mmepitia vipindi tofauti
Katika yote hayo mshukuruni Mungu
Katika yote hayo mshukuruni Mungu
[Chorus]
Kwakuwa amewafikisha hapo mlipo
Kwakuwa amewafikisha hapo mlipo
[Verse 2]
Safari yenu ya ndoa mmeianza kwa imani
Ndio maana mwategemea matokeo mazuri
Yale mtakayotatua mshukuruni Mungu
Na yatakayowashinda mlilieni pamoja
[Verse 3]
Imani yenu yote iwekeni kwa Mungu
Msiweke kwenye vitu, shetani asije ona
Akipigia hivyo vitu, imani itayumba
Imani yenu ikiyumba nanyi mtayumba
[Chorus]
Na ndoa yenu nayo itayumba
Na ndoa yenu nayo itayumba
[Chorus]
Mwende mkaanze maisha
Mungu wenu awalinde
Mbingu zimeshawakubali
Neema iikawafunike
Bwana akawe mwalimu wenu
Akawe mshauri wenu
[Verse 4]
Ndoa ni kama jua lenye mwangaza mwanana
Kila lichomozapo wengi hulifurahia
Watu makundi-makundi hulisifia sana
Jua hili jua zuri lina faida kwa afya
Ila jua lilelile likifika mchana
Wengi hulalamika na kulikimbia
Joto likiwazidia wananung'unika
Joto likiwazidia wananung'unika
[Chorus]
Wanasahau walilisifia asubuhi
Wanasahau walilisifia asubuhi
[Verse 5]
Jua likifika jioni faraja hurejea tena
Ila bahati mbaya, jua laenda kuzama
Hapo sifa za asubuhi huanza kusikika upya
Walovumilia mchana hula matunda yake
Ila tunawaombea Mungu awatetee
Mtakapofika mchana mkavumiliane
Joto likiwazidia mkasemeheane
Msilipize kisasi msije kujidhuru
[Chorus]
Mkakumbuke jioni ya amani yaja
Mkakumbuke jioni ya amani yaja
[Verse 6]
Kama kuna jema lolote msisite kulifanya
Na neno la msamaha msilicheleweshe
Makaishi maisha yenu msiige ya wengine
Epukeni mazoea yanaleta kiburi
Tena maneno mabaya huharibu tabia
Kamwe msije thubutu kuyatunza moyoni
Ndoa ni kipindi cha mwisho cha maisha ya watu
Kitumieni vizuri kwa kuwa ni kifupi
[Chorus]
Maana hamjui lini kifo kitawatenga
Maana hamjui lini kifo kitawatenga
[Verse 7]
Mtendee mema mwenzako kadiri utakavyoweza
Moyo waweza kataa Ila jilazimishe
Kama ukitenda wema huna utakachopoteza
Mtendee akiwa hai macho yake yanaona
Wengi wanajilaumu kuwa walikosea
Wakati wa kutenda wema wao waliumiza
Mungu akawatenganisha, hawaishi pamoja
Wanatamani watende wema Ila walichelewa
[Chorus]
Maana wenzao hawapo tena
Maana wenzao hawapo tena
[Chorus]
Mmeugusa moyo wa Mungu
Kwa kutimiza agano lake
Mungu mbinguni anasubiri oene mtakavyomtukuza
Written by: Ambwene Mwasongwe