Lyrics

Alisikia minon'gono mtaani Watu walikua wakiteta kuhusu yeye, masikini huyu hakujijua Alijiondokea akitikisa kichwa chake Asante sana Bwana umenisaidia, mabaya hayakunikuta mimi Kumbe maneno yale yalikua yake, ila bahati mbaya hakuyajua Alipoyasikia alidhani mapya, kumbe yalikua yanakwisha Alipogundua yanamhusu, alihangaika ajitetee Aliwalaumu sana rafiki zake kwa kujua, wamenyamaza Jamani, jamani Nyamaza, usilie... Mungu atakusaidia, hajawahi kumtupa mtu Nawe hatakutupa, nawe hatakutupa Yakamshinda kuvumilia mabaya yale Kila alipowaona wabaya wake, moyo wake ulipasuka Akapanda gari asijue aendako, njia nzima alikua akiwaza Kwanini Baba yangu, achukue mke wangu Aliwalilia watoto wake, ninawaacha mkiwa wadogo Sikutamani muishi hivyo, ila Mama yenu kasababisha Ninakwenda nikafie mbali, ninasikitika hamtaniona Nisameheni wanangu Sitaki Babu yenu na Mama yenu, waone maiti yangu Mwanangu (mwanangu) mwanangu sikia Unadhani (unadhani) uchungu nilionao moyoni (nilionao) Unaweza (unaweza) kuondoka kwa kuutoa uhai wako? Unadhani utaridhika (kutoa) kutoa, uhai wako Je, pia mwanangu (Je, pia) unadhani Baya (baya-) ulilotendewa unaweza kufutika kwa kulipa kisasi Kwa kulipa kisasi (kwa kulipa kisasi) Malaika wa Bwana walimfuata, alikokwenda Kila alipojaribu kujiua, mara zote hilo lilishindwa Sauti ya Bwana ikasikika ikimwita, rudi nyumbani Ukawaombe msamaha, Baba yako na Mke wako Usiende kuwaambia watoto wako, ubaya wa Mama yao uliotendewa Usije mlaumu Baba yako, mbele ya macho yao wakasikia Mimi nakutuma nina kusudi, ukifika ukawaangukie Nataka nijitukuze kwa nguvu ya msamaha, nenda nipo nawe Usiogope (nyamaza) Nyamaza (usilie) nyamaza, Mungu atakusaidia (Hajawahi) hajawahi, tupa mtu (na hili nalo) Nawe hatakutupa Kwa hili nalo (nawe hatakutupa) Unajua Mungu, unanionea Wamenikosea, hawakuniomba msamaha Nilipoondoka waliniona, japo Watoto wangu na Mama yangu sikuwaaga Iweje leo unambie nirudi, nikawaombe wao msamaha tena Wakati wenyewe walipaswa kuniomba msamaha Ninajua moyo wako, ulivyoumizwa Mwanangu Ndio maana nakutuma, upone Ninakutuma nenda kawaonyeshe, nguvu ya msamaha ah
Lyrics powered by www.musixmatch.com
instagramSharePathic_arrow_out