Lyrics

[Verse 1]
Nakumbuka nikiwa mdogo mimi na ndugu zangu
Siku moja tulikaa mezani
Tulitembelewa na mgeni mwenye rika kama yetu
Akaambiwa aombee chakula
Aliomba maombi mazuri sote tulifurahia
[Verse 2]
Sio kwamba tulikuwa hatuombi tulifundishwa kuomba
Japo tuliomba kwa kukariri
Wazazi wetu waliposikia, waliyapenda maombi yale
Wakatunong'oneza wanawe
Tunataka nanyi muokoke muombe kama hivi
[Chorus]
Hatukujua nini maana yake
Labda kwa kuwa tulikuwa wadogo
Kumbe Mungu anafuatilia
Aliiona shauku ya wazazi
Leo hii tumeshaokokaa
Leo hii tumeshaokokaa
[Verse 3]
Nikikumbuka huwa nacheka wakati mwingine nalia
Njia yangu haikuwa rahisi
Nilisoma sana neno la Mungu nikajitazama nilivyo
Nikajihurumia mwenyewe
Yako wapi matendo ya Mungu yaliyohadithiwa humu
[Verse 4]
Kwa huzuni nikaamua kufunga ili nimuelezee
Nataka kujiuzulu huduma
Kwani majaribu kwangu hayaishi na ninazidi kuchakaa
Ni Bora uwape watu wengine
Mzigo huu ni mzito kwangu kwanza mimi ni mdogo
[Chorus]
Hivi unamgomea nani?
Nimekupa kazi ya kufanya
Ukishinda utavikwa taji
Majaribu kwako ni mtaji
Hebu songa mbele
Hebu songa mbele
[Verse 5]
Sasa nimejua siri za Mungu vile anavyotujali
Yeye huona tusivyoviona
Huviona vikwazo vilivyo mbele hapendi tuangamie
Ndio maana hutuandaa mapema
Tungefukuzaje maadui elfu
Bila kuanza na mmoja
[Verse 6]
Yeye ashikapo kipimo chake apate kutujaribu
Kigezo chake ni uaminifu
Hutumia mambo madogo, madogo
Tuyaonayo halali, ili kupima uaminifu wetu
Angetuwekaje kwenye mambo makubwa
Ikiwa madogo hatuwezi
[Chorus]
Ni jambo moja kumwamini Mungu
Ni kitu kingine yeye kukwamini
Mpaka akuite rafiki yake
Akuonyeshe mbele za shetani
Yahitaji uaminifu
Yahitaji uaminifu
[Bridge]
Nilitiwa moyo na hayo yoote
Nikamwadhimisha yeye
[Chorus]
Ni wewe Bwana (Ni wewe) ni wewe Bwana (Ni wewe)
Uliyefanya haya yote (Ni wewe) uliyeniokoa Mimi (Ni wewe)
Ni wewe Bwana (Ni Wewe)
Ni wewe Bwana (Ni wewe Bwana)
[Outro]
Ni wewe uliyenitoa mbali
Ni wewe uliyenishika mkono
Ni wewe uliyenivusha majaribu
Ni wewe uliyeniinua
Ni wewe Bwana wanguu
Ni wewe uliyefanya yote
Ni wewe Bwana wanguuuu
Ni wewe jemedari wangu
Hallelujah
Written by: Ambwene Mwasongwe
instagramSharePathic_arrow_out