Canciones similares
Letras
[Verse 1]
Ooh sweety, sweety, sweety nisikilize
Sweety, sweety niseme nimalize
Mungu ametukanisha sweet yeeye
Ana maana yake
Mungu katuunganisha sweet wewe
Kwa neema zake eh
I told my mama I want to marry
Nitakuja kwenu nitoe mahali
Mi na we tuanze safari
Ya mbali kina aah
Mbaazi na choroko utofauti utaujua
Jungu kuu wake ukoko yanini kuukwangua
Mie ndama kwako motto
Usije kunikafua
Penzi tulipashe moto
Wakigusa waungua
[PreChorus]
Mithiri ya watoto mapacha tunavyopendana
Mambo ya uzungu na usasa tunayopeana
Penzi twalivujisha pakacha tunavujiana
Wale wenye uchu wa paka hili penzi lawakwama
Baby nasikia twawaumiza
[Chorus]
Pole tunawapa pole
Penzi lawakereketa
Pole tunawapa pole
Ooh hasidi watu wabaya
Pole tunawapa pole
Wameza panadol pengine watapoa
Pole tunawapa pole
[Verse 2]
Eeh
Eeh eeh eeh eeh
Ooh baba ba baba
[Verse 3]
Sweety, sweety, sweety nisikilize
Sweety, ai sweety, nami nikujuze
Eeh shubiri shubiri
Chungu honey
Nashindwa kuficha siri
Yetu ya chumbani
We baba unakidhiri mahabani
Akili yangu na mwili taabani
Eeh
Penzi upepo la pepea (Pepea)
Honey twende mbali (Pepea)
Kuni nitazichochea (Chochea)
Baby uje kupara wali eh
[PreChorus]
Mithiri ya watoto mapacha tunavyopendana
Mambo ya uzungu na usasa tunayopeana
Penzi twalivujisha pakacha tunavujiana
Wale wenye uchu wa paka hili penzi lawakwama
Baby nasikia twawaumiza
[Chorus]
Pole tunawapa pole
Penzi lawakereketa
Pole tunawapa pole
Ooh hasidi watu wabaya
Pole tunawapa pole
Wameza panadol pengine watapoa
Pole tunawapa pole
Written by: Mbosso, Ruby