Lyrics

Wataka akutende nini, akutende nini wee
Wataka akutende nini, akutende nini wee
Ghala lake limejaa, hakuna aliyepunguza hata robo, akutende nini wee
Wengine 'nataka kuwa raisi wa nchi, wengi wataka ubunge, nawe akutende nini wee
Mwingine ombi lake apate shamba, huyu mume na huyu mke, wataka akutende nini wee
Mama huyu ombi lake apate mtoto, mwengine apate elimu, wataka akutende nini wee
Mwambie, mwambie-mwambie
Wataka akutende nini, akutende nini wee
Wataka akutende nini, akutende nini wee
Nakumbuka mgonjwa birikani, miaka thelathini na nane, alikuwa hajiwezi yeye
Yesu akatembelea birika lile, akamwona mgonjwa yule, mara akaanza sababu zake
Malaika akifika anaingia kisimani, anatimua maji, na mimi nakuwa wa mwisho
Eeh, wataka akutendee nini wee
Yesu akasema neno moja, jitwike godoro lako na uende, uendee, mara akawa mzima eeh
Wataka akutende nini, akutende nini wee
Wataka akutende nini, akutende nini wee
Wataka akutende nini, akutende nini wee
Wataka akutende nini, akutende nini wee
Written by: Christina Shusho
instagramSharePathic_arrow_out