Lyrics

Zara Boy pass me the weed I'm about to say something shit nigga Bomboclaat Mh, me nachekaga tu (Mafia) Eh, ukiuliza kiatu ndo kitakwambia Ni mambo mangapi me nimepitia Siwezi rudi nyuma sijakalili njia, yeah Eh, nishakutana na mambo mengi ya dunia Ndo maana hapa nilipo nikikuamulia Hushindi hata ukivaa nguo za kushindia Eeh, hamtaki kutuona mbele kwani wenzetu mnatakaje Tulikotoka tulimwagiwa maji ya maharage Mnatuombea mabaya kwani si tuliwafanyaje Tumekoswa na vibaka mnaomba tuhonge ili tukabe Na kuna vitu mnavifanya bana hamfanyi poa Kwa mawazo yenu mnadhani mnanikomoa Kila nikianzisha penzi mnapanga kulibomoa Au mnataka Yesu arudi anikute bado sijaoa Tuoneane huruma Punguzeni hujuma Wapo wanaotutegemea Nyie mtauwa Tuoneane huruma Punguzeni hujuma Wapo wanaotutegemea Nyie mtauwa Ukidhani unanikomoa mimi Nyuma kuna wengi usiowajua Usiombe wapige goti chini Wakusomee dua men Alhamdulilah Mungu nashukuru Pumzi unanipa silipi ushuru Nipate nikose siwezi kufuru Uzuri umeniumba tembo na sio kunguru Yeah, sina uwoga Me ni maji wasiponinywa watanioga Na wakijisumbua kuniroga Watapoteza muda kama alomtahiri shoga Binadamu bwana eti ye ndo kakupa upofu Na yupo hadharani anasema kuwa uyaone Binadamu bwana Binadamu bwana anaweza kukupa matibabu Na kwenye dua zake anakuombea kwa Mungu usipone Binadamu bwana, eh Tuoneane huruma Punguzeni hujuma Wapo wanaotutegemea Nyie mtawauwa Tuoneane uruma Punguzeni hujuma Wapo wanaotutegemea Nyie utauwa-ah Ukiniletea U-B.I.G nakuletea U-Pac Usinitishie uchawi Me mwenyewe Illuminati Binadamu wana mambo ya kiwaki Unaweza ukang'oka meno wakakuletea mswaki Wakusimama na me wote walikaa Leo wanashangaa ng'ombe wa maskini amezaa Ukinichukia me umeuchukia mtaa Mnaongoja nifeli niko pale nimekaa Tuoneane huruma Punguzeni hujuma Wapo wanaotutegemea Nyie mtauwa Tuoneane huruma Punguzeni hujuma Wapo wanaotutegemea Nyie mtauwa Konde Boy call me number one, number one Is Konde Music Worldwide, mh (Tuoneane huruma) Yeah, we gonna share this message (punguzeni hujuma) To everyone in this world (wapo wanaotutegemea) Me nachekaga tu (Mafia)
Lyrics powered by www.musixmatch.com
instagramSharePathic_arrow_out