Lyrics

(Ndiyo mzee, nimekubali) Naam ndugu wananchi, MC wenu Babu Ayubu Ninawaleteeni habari japo kwa kifupi kuhusiana na huyu mgombea wetu bwana Joseph Haule Mpeni kura za ndiyo kwasababu yeye ni mpenda watu, ni mpenda amani Na ni mtu mwenye huruma kwa wananchi wote Kwa hivyo basi nawaomba ndugu wananchi, mumpe kula ili aingie Naam basi, hivyo basi ndugu wananchi Eeh, tafadhali namkaribisha mgombea wetu Bwana Joseph Haule Ili aje aweza kuzungumza na wananchi, karibu Okay, okay Naitwa Joseph Haule, mwana wa Msulopo Kianzi Nadhani nimeletwa niokoe hiki kizazi Mimi ni mwanasiasa niliyebarikiwa na Mungu Nimeletwa kwenu muungwana niwapunguzie machungu Mimi ni mteule kusini mwa jangwa la sahara Ndiyo maana nimetunukiwa cheti cha juu cha utawala Na hekima kuliko Mfalme Suleiman, msiwe na wasi Na hili nitalidhihirisha pindi mtakaponipa nafasi Actually, nimedhamiria kuwasaidia Taifa lenye nguvu duniani liwe Tanzania Jamani, makofi tafadhali basi jamani! Ni mambo madogo tu Nadhani nitarekebisha mkinipa visiku vichache tu Uchumi utapanda ile ghafla bin-vuu Nataka mpaka Matonya afundishe chuo kikuu Nchi ya Tanzania itang'ara ile kishenzi Na nitahakikisha kila bar-maid anamiliki benzi Si mtafurahi dada zangu jamani? Ndiyo Basi endeleeni kunisifu kwa nyimbo na mapambio Nipeni hiyo nafasi jamani, hamwoni hali ni mbaya? Nataka kuigeuza Tanzania kama Ulaya Cha kwanza nitakachofanya nitafuta umaskini Wanafunzi mkafanyie practical mwezini Kwenye mahospitali nitamwaga dawa kama mchanga Na nitafungua akaunti kwa kila mtoto mchanga Mabomba yatatoa maji na maziwa nchi nzima Watu wa vijijini mtasahau habari za visima Nitafadhili wachawi waweze kutengeneza ndege Kila mtu awe na yake makonda na wapiga debe Si mtafurahi watanzania jamani? Ndiyo mzee Si ni kweli nakubalika jamani? Ndiyo mzee Basi mimi mkombozi wenu jama, ndiyo mzee Na nitafuta shida zenu zote, ndiyo mzee Hivi ni nanii? Ni vijimambo, ndiyo mzee Na vinanikera kweli kweli mimi, ndiyo mzee Basi hali itabadilika sawa? Ndiyo mzee Na hatamu tutaishika okay? Ndiyo mzee Wafanyakazi wa serikalini nashangaa hamna magari Yaani hata mikweche? He-he! Hii ni hatari Ninampango wa kuongeza mishahara iliyo minono Mara mia ya ile ya mwanzo iliyofanya mfanye migomo Nitawapa nyumba nzuri na magari ya kifahari Watu watashangaa mtakapopita kila mahali Mkulima kila mmoja nitampatia trekta Nadhani hiyo kidogo itasaidia kunyanyua sekta Mtauza nafaka zenu bilioni kwa mabilioni Watu midomo wazi kama wamekamatwa ugoni Walimu zawadi zenu oh, nimezificha moyoni Nadhani mtazimia siku mkizitia machoni We acha tu! Mtafurahi nyinyi Ila hapo hapamfai mtu mwingine niwekeni mimi By the way, polisi wote mi' nawasifu Jinsi mnavyokwenda sahani moja na wahalifu Sasa kila mmoja nitampatia helikopta Nadhani hiyo wote hapo hamjawahi kuota Raia wa Tanzania mtalala milango wazi In fact, nina uhakika wa kudhibiti ujambazi Nitajenga barabara tano-tano juu na chini Nitajenga kumbi nyingi sana za starehe baharini Ninaupendo kuliko mshumaa, kumulikia wenzangu Mtakaoyumba kiuchumi, tutagawana vya kwangu Si mtafurahi watanzania jamani? Ndiyo mzee Si ni kweli nakubalika jamani? Ndiyo mzee Basi mimi mkombozi wenu jama, ndiyo mzee Na nitafuta shida zenu zote, ndiyo mzee Hivi ni nanii? Ni vijimambo, ndiyo mzee Na vinanikera kweli kweli mimi, ndiyo mzee Basi hali itabadilika sawa? Ndiyo mzee Na hatamu tutaishika okay? Ndiyo mzee Ndugu wananchi, kuna mtu ana swali kutoka kwa mgombea? Nauliza hivi, kuna mtu ana swali? Basi ajitokeze ili aweze kuuliza swali Nyie ndugu zangu huyu msimpe uongozi, siyo vizuri Muongo tu, mnafiki na kiburi kimsuli Anaongopea sana! Sijui kazaliwa muda gani, alfajiri au alasiri? Au wakati mvua zile, za kipendi kile? Amepita pita school lakini mambo yake si mazuri Wala tusimtetee, atatuangamiza Labda tusubiri kwanza uchaguzi umwekwisha Tumemfuma wenyewe kwa Kalumanzila anasafishwa Kalumanzila akamwambia, "Ehe, shida yako? Elezea fasta fasta kabla jini hajapanda" Hajakaa vizuri mashetani si yakamuanza! Kamsukuma kwa kasi ya kimbunga amejichanja Tulimsikia akisema kwa sauti kubwa ya kukaripia "Waungwana! Munisaidie, Ndiyo, nitamweleza!" Uongo mtupu babake ameibiwa Waungwana wamempeleka jau mpaka kaibiwa Yupo-hamna gepu na bugzi! Amewehuka! Hajatulia huyu mpepeni! Ni sauti iliyosikika kutoka kwa mzee wa pembeni Sijui msaidizi, mganga au mpelelezi Na kwa taarifa yako uongozi hupati ng'o! Labda urudi kwenu uende ukavunje tunguri Na hao waganga wako waeleze hupati kitu apa Hata utoe chapaa Je wananchi mmenisikia? Ndiyo mzee Kwa huyu jamaa hatufai, ndiyo mzee Na inafaa kumchukia, ndiyo mzee Hatumtaki aondoke zake, ndiyo mzee Tusimkubali na maneno yake, ndiyo mzee Tunahakikisha 'atumchagui, ndiyo mzee Kwasab' jamaa ni mnafiki, ndiyo mzee Asitufanye tuwe na dhiki, ndiyo mzee (Ndiyo mzee, nimekubali) (Ndiyo mzee, nimekubali)
Lyrics powered by www.musixmatch.com
instagramSharePathic_arrow_out