Lyrics

[Verse 1]
Ukiona mwanaume kwa hali ya kulia
Jua yakwamba ameguswa pahali
Sio rahisi, si kawaida
Kushuhudia mwanaume akitoa machozi
Hapo zamani nilidhani mwanaume akipoteza kazi ndio uchungu
Ndio unyonge
Kumbe mapenzi ndio sumu kali
Inayofanya mwanaume kulia
Kama mtoto mtoto, kama kidogoyo
[PreChorus]
Hapembelezwi, hanyamazishwi
Machozi yake inatoka ikienda tumboni
Hapembelezwi, hanyamazishwi
Machozi yake inatoka ikienda tumboni
[Chorus]
(Mulika mwizi) Mulika na tochi, mulika
(Mulika mwizi) Kama kuna giza mulika
(Nimulikie mwizi) nasumbuka, nataka kujua nani mwizi wa mapenzi
[Verse 2]
Kwa barua pepe kwa simu ya rununu
Ujumbe mfupi unafutwa na sekundi tatu (Sekundi tatu)
Nilimpenda baibe wangu, nikampea roho yangu
Amechukuliwa, amenyakuliwa
[PreChorus]
Kama fulani hapa mtaani, mwenye magari, na mapesa
Amechukua baibe, ikanifanya crazy
Sipembelezwi, sinyamazishwi
Machozi yangu yanatoka yakienda tumboni
Msiomboleze, mnamujua huyu jamaa
Kajifanya bubu, wengine vipofu
[Chorus]
Mulika mwizi jameni (Mulika mwizi)
Nimulikie mwizi
(Nimulikie mwizi) nasumbuka
Nataka kujua nani mwizi wa mapenzi
Nani mwizi wa mapenzi
[Verse 3]
Ukiona baibe wako anaingia kwa bafu na simu mkononi
Huyo ni mwizi (Mulika mwizi)
Ukiona mzee wako anazima simu kila mara akiwa kwa nyumba
Mulika mwizi (Mulika mwizi)
Oh, oh, oh, oh, ohoo
Oh, oh, oh, oh, ohoo
[Chorus]
Nimulikie mwizi jameni (Mulika mwizi)
(Mulika mwizi) Nionyeshe, niambie ni wapi
(Nimulikie mwizi) mwizi wa mapenzi
Mwizi wa mapenzi (Mulika mwizi)
Nani mwizi wa mapenzi (Mulika mwizi)
Nani mwizi wa mapenzi (Mulika mwizi)
Juu waniua, waniumiza (Ohoo)
(Mulika mwizi) Juu waniumizaa
Oh, oh, oh (Mulika na tochi)
Oh, oh, oh
[Outro]
Natazama mbele si nyuma (Nikiendaa)
Kila mtu mwizi wa mapenzi, kila mtu mwizi wa mapenzi
Pia mimi mwizi wa mapenzii
Written by: Kidum Kibido
instagramSharePathic_arrow_out