Letras

Labda me sijui
Nini mapenzi
Labda me sijui
Nini kupenda
Ila kama hayajakuliza
Kiroho kukuning’iniza
Basi hujapenda
Hauyajui mapenzi
Yatakufanya usilale
Chakula kisipite kwa koo
Kisa mazoea
Wapo waliochanja chale
Kutetea mapenzi
Ila cha ajabu
Cha ajabu
Unayempenda anakutenda
Ila cha ajabu
Cha ajabu
Usiyempenda anakupenda
Kwanza mapenzi konyo
Ona mapenzi sikuelewi
Wanapendwa tu wenye mitonyo
Akina sisi ata kiss hatupewi
Lala lala laaa lalaaa
La la la la la laaa
La la la la la laaa
Naogopa mapenzi mapenzi
Hauyajui mapenzi kama haujawahi pata wivu juu yake
Hauyajui mapenzi kama asiporudi usiku lazima uteseke
Hauyajui mapenzi kama hauyawahi penda usipopendwa mwisho ukaumizwa moyo
Hauyajui mapenzi kama haujasaga meno kulia kisa maumivu ya mapenzi
Ni zaidi ya vidonda mwilini
Utakonda usiamini
Mapenzi
Yatakufanya usilale
Chakula kisipite kwa koo
Kisa mazoea
Wapo waliochanja chale
Kutetea mapenzi
Ila cha ajabu
Cha ajabu
Unayempenda anakutenda
Ila cha ajabu
Cha ajabu
Usiyempenda anakupenda
Kwanza mapenzi konyo
Ona mapenzi sikuelewi
Wanapendwa tu wenye mitonyo
Akina sisi ata kiss hatupewi
Lala lala laaa lalaaa
La la la la la laaa
La la la la la laaa
Naogopa mapenzi mapenzi
Written by: Vii Sugar Boy
instagramSharePathic_arrow_out